ZSSF KUSIMAMIA MIRADI KUWA CHACHU YA UKUAJI WA UCHUMI

MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI YA BLW

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umehimizwa kuendelea kusimamia kwa karibu Miradi mbali mbali ya maendeleo wanayoitekeleza ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwa chachu ya ukuaji wa Uchumi. 

Wajumbe wa kamati ya Bajeti ya Baraza la wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mwanaasha Khamis Juma wametoa maelekezo hayo katika ziara ya kukagua na kupokea Taaarifa ya utekelezaji wa Miradi mbali mbali ikiwemo Kituo cha Mabasi Kijangwani, eneo la maegesho ya Magari Darajani na eneo la Biashara Mbweni ambayo inatekelezwa na Mfuko huo.

Wamesema kukamilika kwa Miradi hiyo itatoa fursa kwa Vijana kupata ajira katika maeneo hayo na kujiongezea pato Binafsi sambamba na ukuaji wa Uchumi. 

Aidha kamati hiyo pia imewahimiza Wataalamu wa mfuko huo kufanya kazi kwa bidii ili kuwapa Wanachama wake huduma zilizobora zinazoakisi kutimiza azma ya Serikali kuwaletea maendeleo Wananchi wake. 

Mkurugenzi Fedha na uhasibu ZSSF Hamad Hamad ameahidi kusimamia maelekezo ya kamati pamoja na kuendeleza juhudi za utafutaji wa fursa mbali mbali za uwekezaji zenye tija ndani na nje ya Nchi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.