Malaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imesema inaendeelea na jitihada za kurudisha huduma ya Maji iliokosekana takriban wiki mbili ndani ya eneo la Mkoa wa Mjini.
Kaimu Mkurugenzi Operesheni ufundi kutoka ZAWA Mhandisi Muhammed Hamdu Haji amesema uharibifu huo umetokana na ujenzi wa miundo mbinu ya Barabara unaoendelea huko kwa Mchina wilaya ya Mjini. Amewataka Wananchi hao kuwa Wastahamilivu kwani mafundi wanaendelea kulifanyia kazi tatizo hilo na wanategemea kumaliza muda wowote kuanzia sasa.
Amewataka Wananchi wenye matatizo mbalimbali ya huduma za maji kufika katika Ofisi zao ili kupatiwa ufumbuzi katika huduma wanazohitaji.
Nao Wananchi wanaokosa huduma hiyo wameiomba ZAWA kuhakikisha wanawatolea taarifa kwa wakati pindi panapojitokeza tatizo pamoja na kuwarudushia huduma hiyo kwa haraka .
Maeneo ambayo yalioathirika kukosa huduma hiyo ni pamoja na Magomeni, Mombasa,Kiembe samaki ,Kwamchina , Kwerekwe, Magogoni, Mpendae na baadhi ya maeneo ya Mbweni