Afisa Elimu Mkoa wa Geita Ndg.Antony Mtweve amezitaka Shule za Serikali na Binafsi kuacha kuchuja Wanafunzi kulingana na ufaulu katikati ya mzunguko wa masomo kwani ni kinyume cha utaratibu wa Serikali na Sera ya Elimu.
Amezungumza hayo wakati akitaja matokeo ya kidato cha nne kwa shule za Serikali na Binafsi Mkoani Geita, huku akisema ufaulu umepanda tofauti na Mwaka jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule binafsi ya Geita Adventist Bi. Bernadeta George amesema moja ya sababu ya kupata ufaulu mzuri katika matokeo ya kidato cha nne Shuleni hapo ni nidhamu.
Makamu Mkuu wa Shule ya Geita Adventist Ndg. Themistocles Chrizostom amesema juhudi kubwa zinafanyika kuongeza ufaulu Shuleni hapo.
Nao baadhi ya Wanafunzi katika Shule hiyo wamezungumzia namna walivyoyapokea matokeo ya kidato cha nne na namna yalivyowapa chachu ya kuongeza juhudi katika masomo.
WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WATAKIWA KUACHA KUCHUJA WANAFUNZI KULINGANA NA UFAULU
stories
standard