JAMII YATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA MALARIA

viongozi wa wizara ya afya wakitoa elimu

      Mashehe na Maimam wamekumbushwa kutoa elimu kwa Waumini wao juu ya athari za ugonjwa wa Malaria ili jamii iweze kuchukuwa tahadhari.

     Akitoa Elimu kwa imam wa Mashehe wa Wilaya ya Mjini Afisa kitengo cha malaria Ndg.Mwinyi Khamis amesema kumekuwa na ongezeko la ugonjwa huo na tayari baadhi ya watu wamepoteza maisha.

     Ndg.Mwinyi amesema elimu hiyo ni muhimu kwa Viongozi hao wa Dini kutoa elimu kwa waumini wao ili kuwa na njia za kujikinga,

amesema mtu  atakaeona dalili za ugonjwa huo ni vyema kupata tiba sahihi kusudi kuondosha ugonjwa huo.

       Nao  Maimamu wamekubali kuchukuwa dhamana ya kutoa uelewa kwa Waumini wao.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.