WAANDISHI WA HABARI KUVITANGAZA VIVUTIO VYA UTALII PEMBA.

WAANDISHI WA HABARI PEMBA

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kutumia nafasi yao katika kuvitangaza vivutio vya utalii Kisiwani humo ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali kukifunguwa  Kisiwa hicho Kitalii na kuimarisha uchumi wa Nchi.

Ushauri huo  umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la Kihistoria huko Chwaka Tumbe  ikiwa ni ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Utalii na mambo ya kale kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa habari  Kisiwani Pemba .

Amesema  ni vyema waandishi wa habari  kuwapatia Wananchi  Taarifa sahihi  juu ya  maendeleo makubwa yaliyopatikana Nchini,kupitia Sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Utalii pamoja na kuunga Mkono juhudi hizo ili kuweza kupiga hatua zaidi za Kimaendeleo.

Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na mambo ya kale  Zuhura Mgeni Othman  amesema Sekta ya Utalii ni Sekta Mtambuka ambayo inachangia kwa kiasi  Kikubwa  Pato la Taifa  hivyo  ziara hiyo  kwa Waandishi Wahabari  kuvitangaza vifutio hivyo  na kutowa Taaluma Wananchi waweze kuvitembelea  kwa lengo la kujua Historia yao pamoja na kuchangia pato la Taifa ili malengo yaweze kufikiwa.

Nae Mwenyekiti wa Club ya Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba Bakar Mussa Juma amesema Dhamira ya Club hiyo ni kuunga Mkono Utalii wa ndani na kuvitangaza Vivutio vya Utalii Kisiwani humo ili kuweza kukifunguwa Kiutalii na kuenuwa Uchumi.

Kisiwa cha Pemba kimebarikiwa kuwa na  vivutio vingi vya Utalii ambavyo  Takribani  vivutio 45 tayari vimekwisha kutambulika rasmi ikiwemo Mkamandume,Rasi mkumbuu ,Chakwa Tumbe  na 15  bado vinaendelea  kufanyiwa utafiti wa awali  huku Mkoa wa Kaskazini Pemba ukitajwa kuongoza kwa maeneo mengi ya Kiutalii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.