SUALA LA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI LINAHITAJI MUDA

ZPRA

  Mamlaka ya utafutaji na uchimabaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar imesema suala la utafutaji wa rasilima hizo unahitaji utafiti wa kina ili kukamilika kwake na kupata matokeo sahihi kwa zoezi hilo.

      Wakitoa uwelewa kwa Watendaji wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar kuhusu hatua iliyofikia Mkurugenzi idara ya data Ndg.Mohamed Salum na Meneja wa mamlaka hiyo Ndg. Khamis Juma wamesema hadi sasa kumetangazwa uwepo wa vitalu na maandalizi yake ni kuvitangaza kwa ajili ya wawekezaji kuekeza.

       Mkurugenzi idara ya mipango na masoko Shirika la Mawasiliano Zanzibar Ndg.Abubakar Ali Sheha amesema bado juhudi zinahitajika kwa ZPRA katika kutoa uwelewa kwa Wananchi ili ufahamu kuhusu uwepo wa Mafuta na gesi.

      Nao Watendaji wa Shirika hilo wamesema elimu iliotolewa imeongeza ufahamu na hatua inayoendelea ya mafuta na gesi asilia ni kuhakikisha kuwa elimu hiyo wataifanyia kazi kwa wengine.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.