ZECO YAJIPANGA KUONDOA KERO YA UMEME

ZECO LAINI MPYA ZA UMEME

    Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) linajenga laini mpya kutoka Mtoni kwenda vituo vyengine ili kuondokana na  tatizo la kukatika ovyo kwa umeme kwa baadhi ya maeneo.

      Akizungumza wakati mafundi wa ZECO wakiendelea na matengenezo kwa laini ya Dole na Maruhubi, Mhandisi ugavi wa Shirika Ndg. Ali  Kassim Fumu, amesema kumekuwa na jitihada ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kwa kipindi kifupi kijacho.

     Amafahamisha kuwa hali inayosababisha maeneo hayo kukosa huduma kwa uhakika ni kuzidiwa kwa laini kubwa zinazosafirisha umeme eneo la Dole na Maruhubi.

      Ameyataja maeneo ambayo yanakatika umeme mara kwa mara ni pamoja na Ddole, Mwanyanya, Kianga, Miwani, Masingini, Kibweni, Bububu, Mtoni na Maruhubi.

     Naye Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa shirika hilo, Ndg. Haji Juma Chapa, amesema katika kuimarisha huduma hiyo, ZECO imedhamiria kuwa na ujenzi na uzalishaji wa nishati mbadala ili kuondosha tatizo la kuzidiwa kwa laini hizo.

      Nao baadhi ya Wananchi wa maeneo ya Mwanyanya, wameelezea kufarajika na upatikanaji wa huduma hiyo kwa kiwango cha uhakika tofauti na hapo awali.

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.