Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Omar Haji Gora ameitaka Jamii kuhakikisha wanapiga vita suala la udhalilishaji kwa Wanawake na Watoto ambalo linaleta athari katika Jamii .
Akifungua mafunzo ya ushauri nasaha kwa wahusika wa masuala ya udhalilishaji Gora amesema endapo juhudi zitachukuliwa tatizo hilo linaweza kuondoka na kupatiwa ufumbuzi katika Jamii.
Naibu Katibu Gora amewaomba wasimamizi kusimamia kesi hizi kwa uadilifu ,na uaminifu na kuitaka Jamii kufata utaratibu Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ili kujua muendelezo wa kesi unavoendelea.
Mkurugenzi Katiba na msaada wa kisheria Hanifa Ramadhan Said amesema lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na kushirikiana na kuwasadia katika afya ya akili kwa kuwasaidia kutokata tamaa mapema.
Muwasilishaji wa mada ya ushauri nasaha juu ya masuala ya udhalilishaji Asaa Jaffar Omar kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto amewataka Wazazi kuwa karibu na Watoto wao na kuwafatilia nyendo zao na ili wanapopata tatizo waweze kukueleza kwa wakati.