BODI YA VILEO YATKIWA KUONDOSHA KASORO ZA UTOAJI WA HUDUMA KWA WAGENI

WAZIRI WA UTALII  PAMOJA NA WADAU SEKTA UTALII

   Wizara ya Utalii na mambo ya kale Zanzibar imeitaka bodi ya vileo kuondosha kasoro zilizopo katika utoaji wa huduma kwa wageni ili kulinda biashara ya utalii.

   Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Simai Mohamed Said ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya utalii huko Kikwajuni Mjini Zanzibar ambapo amesema uwepo wa kasoro katika sekta hiyo unaweza kuathiri harakati za uchumi ambao kwa kiasi kikubwa unategemea sekta ya utalii.

   Hata hivyo Mhe. Simai amewaomba wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo wawekezaji kutoka nje ya nchi kuendelea kuwa wavumilivu huku serikali ikilitafutia ufumbuzi jambo hilo.

   Hivi karibuni bodi ya vileo imefanya maamuzi ya kubadilisha mawakala ambao wanaleta vinywaji kutoka Tanzania Bara na Nje ya Nchi , Hatua ambayo kwa sasa imeanza kusuasua hali inayopelekea hoteli nyingi kukosa huduma hiyo katika maeneo mbali mbali. 

 

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.