WAMILIKI NA WALIMU SHULE BINAFSI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA

WIZARA YA ELIMU NA WAMILIKI WA SHULE BINAFSI

   Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zaznzibar Mh. Leila Mohamed Mussa amewataka wamiliki na walimu wakuu wa shule binafsi kisiwani Pemba kuhakikisha wanashirikiana na Wizara katika kupanga mipango yao ya kitaaluma.

   Waziri Leila ametoa wito huo huko katika ukumbi wa Chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji Chakechake Pemba alipokutana na wamiliki  hao pamoja na walimu wa shule hizo kwa lengo la kujadiliana juu ya msauala mbalimbali ya maendeleo ya elimu katika sekta binafsi.

    Amesema shule zote zile za serikali na binafsi zina mchango mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya kieleimu Visiwani hapa , Hivyo kila uapande unatakiwa kutimiza majukumu yake.

     Akizungumzia mchango wa shule binafsi Kisiwani Pemba Afisa elimu Mkoa wa Kusini Pemba Ndg. Mohamed Shamte ,Amesema shule binafsi zina mchango mkubwa lichja ya kuwepo baadhi ya changamoto.

  Kwa upande wao baadhi wa wamiliki na walimu wakuu wa shule za binafsi  Pemba wameeleza baadhi ya changamoto zao.

Mkutano huo ni program maalum za uongozi wa Waziri wa elimu na Mafunzo ya amali kukutana na wadau wa elimu kujadili maendeleo ya elimu Visiwani Zanzibar.

 

 

 

 

 

 

standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.