Dk. Samia Ameyasema Hayo Katika Ziara Yake Ya Kichama Katika Mkoa Wa Kaskazini Unguja, Wakati Akifungua Tawi La CCM Chaani Masingini Na Kufungua Kituo Cha Ushoni Cha Wanawake Mahonda, Amesema Viongozi Ambao Wapo Nyuma Kikazi Hawana Budi Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Kipindi Kilichobaki.
Rais Samia Amewataka Wanachama Na Wananchi Wanapokwenda Kupiga Kura Kuhakikisha Wanawapima Viongozi Kwa Kazi Walizozifanya Na Kuacha Mtindo Wa Kupewa Rushwa, Ikiwemo Kanga Na Pesa Kwa Ajili Ya Kuwapa Kura Kwani Anaefanya Hivyo Hakufanya Kazi Yake Kwa Umakini.
Hata Hivyo, Rais Samia Amesema Wanaccm Ndio Wenye Serikali Kwani Waliokuwepo Juu Ndio Watu Walioaminiwa Kuwaongoza Katika Ngazi Mbalimbali Kwa Serikali Zote Mbili Za Tanzania.
Baadhi Ya Viongozi Wa Mkoa Wa Kaskazini Unguja Wamefurahishwa Na Kauli Ya Mwenyekiti Huyo Juu Ya Kuwapima Viongozi Na Kuahidi Kuendelea Kuwaletea Maendeleo Wananchi Hasa Wanawake Ili Kujikwamua Na Umaskini.
Nae Mhe. Zainab Shomari Amesema Mkoa Wa Kaskazini Unguja Unatekeleza Kwa Vitendo Ahadi Za Chama Cha Mapinduzi Ambapo Kuwepo Kwa Chuo Hicho Ni Kuwawezesha Wanawake Kujiajiri Wenyewe.