JUMLA YA WATU 15 WAMEOKOLEWA NA MMOJA KUJERUHIWA KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO LILILOKUWA LIKIFANYIWA MATENGENEZO KATIKA ENEO LA FORODHANI

ajali

Katika Ajali Hiyo Iliyotokea Majira Ya Mchana, Jengo Hilo Lililoporomoka Ambalo Lilikuwa Benki Ya PBZ, Lipo Katika Matengenezo Na Wakati Ajali Inatokea Watu 16 Walikuwemo Ndani Ya Nyumba Hiyo, Majeruhi Ambae Alifunikwa  Akitambuliwa Kwa Jina La Mayani Mussa Bakari  Anasadikiwa Kuwa Na Miaka 35 Aliokolewa Kwa Msaada Wa Kikosi Cha Zimamoto Na Uokozi.

 

Akizungumzia Tukio Hilo Mkuu Wa Operation Kikosi Cha Zimamoto Na Uokozi Mrakib Mbarouk Ali Juma Amesema, Wamefanikiwa Kufanya Uokozi Huku Akitoa Wito Kwa Wananchi Kutokuwa Karibu Na Jengo Hilo Ili Kuepusha Athari Zaidi.

 

Nao Mashuhuda Wa Tukio Hilo Wamesema Wameshuhudia Jengo Likianguka Na Kutoa Taarifa.

 

Kufuatia Ajali Hiyo Viongozi Mbalimbali Wamefika Eneo La Tukio Kufuatilia Kwa Karibu Hali Iliyopo Na Namna Mamlaka Zinavyoweza Kujipanga Na Kuchukuwa Hatua.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.