Ameyasema hayo Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dk Philip Isdor Mpango wakati wa uzinduzi wa Skuli Ya Elimu Mjumuisho-Jendele Dk Mpango Amesema Mapinduzi Ya Zanzibar Yameiletea Heshima Kubwa Zanzibar Ambapo Sekta Ya Elimu Imepewa Umuhimu Na Kuweka Usawa Katika Upatikanaji Wa Elimu Ikiwemo Mjumuisho
Dk Mpango Amewaomba Wananchi Kuitumia Fursa Ya Kuanzishwa Skuli Hiyo Ya Elimu Mjumuisho Kwa Kutowaficha Watoto Wenye Ulemavu Kwani Serikali Zote Mbili Zitaendela Kuipa Umuhimu Sekta Ya Elimu Kwa Kuweka Mazingira Mazuri Ya Upatikanaji Mikopo Ya Elimu Ya Juu Kwa Vijana
Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Mhe Leila Mohamed Mussa Serikali Imevuka Malengo Ya Utekelezaji Wa Miradi Ya Elimu Na Itaendelea Kuweka Mazingira Bora Ikiwemo Maslahi Ya Walimu Na Vifaa Vya Kisasa.
Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Amali Bw Khamis Abdalla Said Amesema Ujenzi Wa Skuli Ni Juhudi Za Serikali Kuhakikisha Elimu Ya Lazima Inatolewa Kwa Makundi Yote Ambapo Kiasi Ya Shilingi Bilioni 3 Nukta Saba Zimetumika