CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KITAENDELEA KUWAMINI VIJANA KAMA NYENZO MUHIMU YA UTAYARI KATIKA MAENDELEO NA MIPANGO YA SERIKALI.

RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan  amesema Chama hicho kitaendelea kuwamini Vijana kama nyenzo muhimu ya utayari katika Maendeleo na Mipango ya Serikali.

Mwenyekiti huyo wa CCM ambae ni Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza baada ya kupokea matmbezi ya umoja wa Vijana wa CCM ikiwa ni kilele cha matembezi hayo huko maisra, amesema kwa msingi huo Vijana wanapaswa kujengewa uwezo pamoja na kuendeleza vipaji vyao huku akiwataka kujitambua.

Aidha Mwenyekiti huyo, amewahimiza Vijana matumizi sahihi ya Mitandao, na waitumie kwa tija ili kuzibaini fursa zinazopatikana kupitia mitandao hiyo.

Naibu Katibu Mkuu CCM  Zanzibar Mohamed Said Dimwa amesema ni vyema Vijana wakaelewa sababu ya kufanyikaa Mapinduzi na kuahidi kuyaenzi kwa kuleta mshikamano na maendeleo.

Mohamed Ali kawaida Mwenyekiti wa UVCCM Taifa ameahidi kuwa Vijana kupitia umoja huo wataendelea kuwa Wazalendo na kushirikishwa katika masuala mbalimbali.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.