Kampuni ya ujenzi ya Serikali ya China CCECC imesema itaendelea kutekeleza maagizo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha Miundombinu ya usafiri ili kuondoa tatizo la Miundombinu liliopo Nchini.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya CCECC Tanzania na Afrika Mashariki Zhang junle akizungumza na waandishi wa habari huko Serena Hotel amesema Serikali ya China inaipongeza SMZ kwa kuendelea kuiyamini katika ujenzi wa Miradi ya Barabara inayoendelea na kuahidi kumaliza kwa wakati
Akizungumzia ushiriki wa wazawa katika fursa za ajira amesema Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara hizo unahusisha matumizi ya Wataalam wa ndani kwenye kubadilishana ujuzi na Vifaa hali inayopunguza ukosefu wa ajira
Urafiki wa China na Zanzibar ulianza tangu Mwaka 1964, baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomuondoa Sultani Jamshid Bin Abdullah. China ilikuwa Nchi ya kwanza kutambua na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Zanzibar.