WATOTO WASISITIZWA KUWA MAKINI NA ATHARI ZA MVUA

Pemba

     Watoto wa kijiji cha Uwandani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kuzingatia usalama wao kwanza katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha hasa wanapokwenda mtoni kwa ajili ya kuogelea na kucheza ili kujiepusha na madhara yanayosababishwa na mvua hizo.

     Kauli hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Shaaban Nassor ambae pia ni Mkaguzi wa Shehia hio wakati alipokuwa akipita katika maeneo mbalimbali katika Shehia yake kusikiliza changamoto za wananchi ambapo moja kati ya changamoto aliyoipata ni watoto kucheza katika maeneo ambayo maji yanatuwama kwa kiwango kikubwa jambo ambalo ambalo kama watoto hawatadhibitiwa ipasavyo inaweza kusababisha madhara.

      Akizungumza na watoto hao aliwataka kuacha tabia ya kucheza na kuogelea katika maeneo ya mito yenye maji mengi kwa kuwa maeneo hayo sio salama kwao.

     Aidha Mkaguzi huyo aliendelea kutoa elimu kuhusu madhara yanayoweza kuwapata watoto hao endapo wataendelea kucheza katika maeneo hayo.

     Akiyataja madhara yanayoweza kuwapata ni pamoja na kuzama, kunasa kwenye tope na kupata maradhi ya mripuko wa magonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo.

     Sambamba na hayo amewataka wazazi waelewe kuwa usalama wa watoto unaaza na mzazi hivyo ni wajibu wao kuwasimia na kuwalinda ili wasipate madhara hasa katika kipindi hichi cha mvua.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.