UAMINIFU NA UADILIFU KATIKA KAZI ZA UCHUNGUZI (MAABARA) HUMTOA MWANANCHI WASIWASI KWA KUPATA MAJIBU SAHIHI

Maadhimisho ya siku ya vinasaba nchini

      Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka Mawakala wa Maabara ya Serikali kuendelea kuwa waaminifu na waadilifu katika kazi zao za kiuchunguzi wa matatizo ili wananchi waamini majibu yanayotolewa na taasisi hiyo.

       Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Shekh Idriss Abdul-wakil Kikwajuni katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Vinasaba Duniani.

      Amesema kuwa uaminifu na uadilifu katika kazi za kiuchunguzi ni njia moja wapo inayowafanya wananchi kutokuwa na wasiwasi kwa kupata majibu sahihi na kuamini kile wanachoambiwai.

        Amesema kuwa vinasaba ni huduma muhumu sana katika kuchunguza jambo ama kwa binadamu au hata katika kilimo ambapo vinasaidia kubainisha tatizo na oweza kutengeneza dawa.

       Aidha amefahamisha kuwa watoto wengi wanaozaliwa Zanzibar wanaugua maradhi ya .mifupa kutokana na ukosefu wa upimaji wa vinasaba kabla ndoa jambo ambalo ni kikwazo.

       Ameeleza kuwa maadhimisho ya siku ya vinasaba duniani yametangazwa rasmi na Baraza la Seneta la Marekani ambapo baraza hilo limeitaka dunia kuadhimisha siku hiyo kila mwaka.

       Katika hatua nyingine Waziri Mazrui amewasisitiza wanafunzi kusoma sana masomo ya Sayansi ili kusaidia Serikali katika kufanya utafiti na kujua vinasaba kupitia makundi mbalimbali ikiwemo kilimo, afya na wanyama.

      Akitoa salamu za Wakala wa Maabara ya Serikali Mkemia Mkuu wa Serikali Faridi Mzee Mpatani amesema kuwa teknolojia ya vinasaba inasaidia kutatua matatizo mengi yanayotokea katika jamii na kutafutiwa ufumbuzi kwa mujibu wa sheria.

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.