SMZ NA SAUDIARABIA KUENDELEZA USHIRIKIANO

Dkt.Mwinyi

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi  ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi ya maendeleo.

    Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania, Yahya Ahmad Okeish na Ujumbe wake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Nchi mbili hizo.

     Rais wa Zanzibar amesema, Zanzibar ni mnufaika mkubwa wa mfuko wa Saudia na Quwait kwenye miradi yake ya maendeleo kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya Mataifa hayo.

    Balozi Okeish amepongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Zanzibar na Tanzania kutimiza Miaka 60 ya Muungano na kuuombea mafanikio zaidi muungano huo huku akisifu ushirikiano wa Diplomasia uliopo pamoja na utamaduni za pande mbili hizo.

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.