KAZI YA UHAKIKI INAFANYIKA KWA UFANISI LICHA YA KUWEPO KWA ONGEZEKO LA IDADI YA WASTAAFU MWAKA HUU.

ZSSF

Akizungumza katika zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa Pencheni zao na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), linalofanyika kituo cha Kitogani kwa siku mbili, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  kutoka ZSSF, Raya Hamdani amesema hadi sasa kiasi ya wastaafu elfu tisa wameshafanyiwa uhakiki kati ya wastaafu elfu 13 na mia tano  wanaowatarajia kuwafanyia uhakiki huo, huku akiwaomba wastaafu wote ambao hawatohakikiwa katika kipindi hiki kufuata huduma hiyo makao makuu ili kuepuka usumbufu.

Baadhi ya wastaafu wameeleza kuridhishwa na utaratibu wa uhakiki na kuuomba Mfuko wa Hifadhi ya Jamii  (ZSSF), kuweka utaratibu maalum wa kutoa taarifa wakati pencheni zao za kila mwezi zinapokuwa tayari.

Uhakiki wa wastaafu wa ZSSF mwaka huu limeanza tarehe 2  katika vituo mbali mbali Unguja na Pemba na linatarajiwa kukamilika leo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.