BARABARA YENYE UREFU WA KILOMITA 2.4 KUFUNGULIWA

 Mhe. Masoud

Waziri  wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohamed ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi inazozichukua katika kuimarisha ujenzi wa miundombinu ya barabara.   

Mhe. Masoud ameeleza hayo wakati akiizindua rasmi barabara ya Mgeni Haji-Kwambani yenye urefu wa kilomita 2.4.

Amesema juhudi zinazochukuliwa na Serikali wananchi wanapaswa kuzilinda na kuzitunza barabara  ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

Mhe. Msoud amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa usimamizi mzuri katika kuhakikisha barabara nyingi zinajengwa kwa wakati mmoja.     

Akitoa taarifa ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Shomari Omar Shomari amesema ujenzi wa barabara hiyo ni miongoni mwa ujenzi wa barabara za kilomita 275.9 ambazo zinajengwa unguja na pemba.    

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.