Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa takwimu ya mwezi Julai 2024, Mwaka wa Fedha 2024/25 kuwa imefanikiwa kukusanya Tsh. trilioni 2.34, sawa na ufanisi wa 104.4% ikilinganishwa na lengo la kukusanya Tsh. trilioni 2.246
Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa 20% ikilinganishwa na Tsh. trilioni 1.94 zilizokusanywa katika mwezi Julai kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, August 10, 2024 imesema
“Ufanisi katika makusanyo na ukuaji wa makusanyo kwa mwezi July ni wa juu kabisa kufikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kipindi cha miaka sita iliyopita”-Mwenda.
stories
standard