MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO IMEHAMISHIWA OFISI YA RAIS IKULU

MHE ALI SULEIMAN AMEIR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amewataka Viongozi na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao kuhakikisha kuwa inayaendeleza mazuri yaliyokuwa yakifanyika kabla ya kuhamia Ofisi ya Rais Ikulu.

Waziri Mrembo ameyasema hayo huko Mazizini alipokuwa akijitambulisha Rasmi kwa Viongozi na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Serikali mtandao baada ya Mamlaka hiyo kuhamishwa kutoka Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora na kuingizwa katika usimamizi wa Ofisi ya Rais Ikulu. 

Mhe. Waziri amewataka Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuendeleza yaliyokuwa yakifanyika kabla ya kuhamia Ofisi ya Rais Ikulu pamoja na kuzitatua maeneo ambayo yaliyokuwa na matatizo ya Kiutendaji.

Amesema Serikali ina mategemeo kutoka kwa Mamlaka hiyo, hivyo Wafanyakazi hao Watumie weledi kufikia Malengo ya Serikali huku akiwasisitiza suala la ulinzi na uhifadhi wa taarifa muhimu za mitandao.

Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Saleh Juma Mussa amesisitiza Uzalendo kwa Wafanyakazi, Heshima baina ya Wafanyakazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Said Seif said amewashukuru viongozi hao wa ofisi ya rais ikulu kwa kufika katika Ofisi ya Mamlaka na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yaliyotolewa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.