Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan Amewaongoza Viongozi mbalimbli akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Waliopigania Uhuru wa Tanzania katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Aidha Rais Samia ameweka Mkuki na Ngao katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa hao akiwemo Mkuu wa Majeshi,Brigedia Jenerali Mkunda ambaye aliweka Sime.
Baadhi ya Mashujaa Walioshiriki katika Vita akiwemo Brigedia Jenerali Mstaafu Simba Waziri Simba ambaye aliwaakilisha Wapigania Uhuru na Kupigana Vita ya Kagera Mnamo Mwaka 1978 Hadi 1979 ameeleza namna alivyotekeleza Majukumu yake.
Nao baadhi ya Wananchi wametoa Maoni yao kuhusiana na Siku ya Mashujaa ambapo wamewahimiza Vijana kujitokeza kwa wingi kwenye Siku kama hizo ili kuendelea kujifunza yale yaliyofanywa na Mashujaa wa Nchi.