Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira na Bodi ya Maji, Bonde la Wami Ruvu kushirikiana kuondoa Majani ambayo yaliyoota juu ya Maji ya Bwawa la Mindu lililopo Manispaa ya Morogoro ambalo linategemewa na wakazi wa Manispaa hiyo.
Mheshimiwa Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa Ziara yake ya Siku Moja Mkoani morogoro ya kutembele Bwawa hilo na kushuhudia Majani ambayo yameota juu ya Maji huku shughuli za kuyaondoa zikiendelea.
Aidha Waziri Aweso wakati akiongea na Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira (Moruwasa) amelazimika kumsimisha kazi mtumishi wa Moruwasa baada ya baadhi ya maeneo yakiwemo Tungi na Nanenane Manispaaa Morogoro kushindwa kupata Maji kwa Wiki Tatu.
stories
standard