SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU NA WAFADHILI WA NDANI NA NJE YA NCHI

MH LEILA MOHAMMED MUSSA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Leila Mohammed Mussan amesema wataendelea kushirikiana na Wadau na wafadhili wa ndani na Nje ya Nchi kwa lengo la  kukuza Sekta za Elimu ya juu   ili kupata Wataalamu wa baadae.

Akizungumza na Wadau mbalimbali huko  Chuo iit Madrasa Compas Bweleo amesema ushirikiano huo itasaidia kupiga hatua  za kimaendeleo na kutoa fursa kwa Vijana wasomi  ili kujikuza Kielimu na kuiletea Mandeleo Serekali na kuwasisitiza  Wanafunzi wa chuo hicho  kuongeza  juhudi  katika masomo yao ili Wadau hao waweze   kuwaunga Mkono

Nao Wadau hao wamesema  Wataendendeleza ushirikiano   na kukisaidia Chuo hicho pamoja na Wanafunzi hasa wale wenye uwezo mdogo ili kujiendeleza Kielimu

Zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili za Kitanzania zimetolewa na Kampuni mbalimbali  kwa ajili ada ya Wanafunzi na maendeleo ya Chuo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.