Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi Mkoani Rukwa kutunza Miradi inayojengwa kwenye Maeneo yao ili iweze kudumu na kuleta tija ya fedha zinazotumika kukamilisha Miradi hiyo.
Hayo yamejiri wakati wa Ziara ya Kikazi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkoani Rukwa,ambapo amezindua Hospitali ya Wilaya ya Nkasi iliyoghalimu kiasi cha Fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 5 na kuwataka Wananchi kuthamini na kutunza miundombinu ambayo Serikali imnekuwa ikitumia gharama kubwa kwa ajili ya Manufaa yao.
Baadhi ya Wanachi waliofika kushuhudia ujio wa Rais Samia Mkoani Rukwa wakati wa Uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa namna ambavyo imekuwa imara katika kutekeleza Miradi mbalimbali.
Rais Samia anaendelea na Ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Rukwa Mkoani Rukwa kwa Muda wa Siku Tatu.