Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya imeteketeza Dawa za Kulevya aina mbalimbali ikiwemo Heroine, Bangi, Mirungi na Valiamu.
Akizungumza katika zoezi la uteketezaji wa Dawa hizo huko Mahonda kamishna wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Kanali Burhani Zuberi Nassor amesema Dawa hizo ambazo kesi zake zimeshaisha tokea Mwaka 2018 hadi 2024 na wanaokamatwa na Dawa hizo mali zao zinataifishwa.
Amesema mapambano bado yanaendelea ya kufanya utafiti kujua kiwango gani ambacho kiloopo na wanachi na kiwango gani wamefaulu na kujua wapi wamefiko kwa sababu zanziar ni kisiwa ambapo Bandari Bubu 370 zipo hivyo hupelekea kupata ügümü katika napambano hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe Harous Said Suleiman amesema Serikali itaendelea na kulifanya zoezi hilo likiwa na lengo ni kuona Dawa zilizokamatwa hazirudi Mitaani na kuwataka Wananchi kushirikiana na serikali ili kuwadhibiti wanaoingiza Dawa hizo Nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira Sheha Mjaja Juma amesema zoezi hilo haliwezi kuleta athari kwa Jamii kwani limeefanyika kwa umakini.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya kusimamia Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi ya Mhe Machano Othmani Said amesema Kamati yake itaishauri mamlaka kuzichoma Dawa hizo kwa kila Mwaka mara moja au Mbili ili kuepusha kupotea kwa vielelezo.