VIONGOZI WA DINI WAMETAKIWA KUHUBIRI AMANI.

NAIBU KADHI MKUU ZANZIBAR

Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Othman Ame Choum amewataka Viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri Amani kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta maedneleo Nchini.

Naibu Kadhi huyo ameseyasema hayo huko Gombani katika Kongamano la

Kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1446 Hijria ,lililowakutanisha Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamiu .

Amesema suala la uvunjifu wa Amani silakupewa nafasi kutokana na kuwepo kwa Athari kubwa katika Jamii kiuchumi na Kimaendeleo hivyo ni jukumu la Waislam  Kuendelea kutunza amani kwa faida yao na Taifa.

Nae Mratibu wa Ofisi ya Mufti Pemba Shekhe Said Ahmad amesema ikiwa tunaelekea

Mwaka mpya wa Kiislamu ni vyema kwa Waumini wa Dini hiyo kujitathmini na

Kuendeleza upendo na Amani katika Jamii zao ili kuwa na nafasi kubwa ya kumcha Mungu na kuweza kufanyashughuli za uzalishaji kwa lengo la kupata Maendeleo.

Akitowa mada katika kongamano hilo shekhe ali hilali ali ameipongeza serikali kwa kuona thamani ya Mwaka mpya wa Kiislamu ,huku akielezea kuwa tarehe ya Kiislamu

Ni muhimu kuzijuwa kwani ndio dira ya maendeleo katika Maisha ya Mwanadamu. 

 Mapema akizungumza katika Kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amesema Viongozi wa Dini Wananafasi kubwa katika Serikali na Jamii hivyo ni wajibu wao kuona Wanahamasisha Jamii kuishi kwa utaratibu wa miongozo ya Kidini kwa kuweza kuondoa Vitendo viovu na kuwa na Jamii bora.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.