ZANROAD NA TANROAD YAINGIA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO KATIKA KAZI

UTIAJI SAINI

   Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Barabara Zanzibar Yasser De Costa amesema ushirikiano wa Wakala wa Barabara Zanzibar na Wakala wa Barabara Tanzania utasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

    Kauli hiyo ameitoa wakati wa utiaji Saini wa makubaliano ya mpango kazi ya utekelezaji kwa Watendaji wa Zanroad na Tanroad huko katika Ofisi za Tanroad Dare-salam na kuwataka Watendaji hao kuhakikisha wanayafuata maelekezo waliyokubaliana ili kufikia lengo.

    Aidha amefahamisha kuwa ushirikiano huo kutaimarisha utendaji kazi kwa kuweka mikakati ambayo itakua rafiki kwao na kutoa matokeo mazuri kwa serekali.

    Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Barabra Zanzibar Mhandisi Cosmas Masolwa na Mwakilishi wa Wakala wa Barabara Tanzania Mhandisi Peter Bululu wamesema kukamilika kwa Utiaji Saini huo kutasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.