WANANCHI WA KIJIJI CHA UZI WATAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO KWA POLISI JAMII

WANANCHI WA KIJIJI CHA UZI

   Mkuu wa Wilaya ya Sadifa Juma Khamis , amewataka Wananchi wa Kijiji cha Uzi kutoa ushirikiano wa dhati na Askari Jamii wa Shehia hiyo ili Kisiwa hicho kiendelee kubaki salama pamoja na Wakaazi wake.

    Amesema hayo huko katika Kijiji cha Uzi, katika Sherehe ya kuwapongeza Askari Jamii kwa kazi  ya kupunguza Vitendo viovu vikiwemo vya Wizi, amesema ni hatua nzuri iliyofikiwa kwa sasa, hivyo amewasisitiza Askari hao kutochoka kuwakabili wale wanaorudia au kujaribu kufanya vitendo visivyo halali.

   Akisoma Risala  ya Askari Jamii wa Shehia ya Uzi,  Badru Aboud Salum, amesema wamefanikiwa kwa Asilimia 75, ambapo wameweza kudhibiti vitendo vya uhalifu Wizi wa Mazao na Mifugo, Dawa za Kulevya, Biashara ya Ngono, uharibifu wa mazingira pamoja na Vitendo vya udhalilishaji 

   Aidha amesema kuwa wanakabili na tatizo la kubezwa na kudharauliwa na baadhi ya Wananchi wa Kisiwa hicho, uhaba wa vitendea kazi ikiwemo Pingu, Rainboot, Tochi na Vifaa vyengine vinavyohusiana na Kazi zao.

    Mkuu wa Polisi  Wilaya ya Kati amesema watahakikisha wanawaunga mkono  ili kuhakikisha vitendo vyote viovu vilivyodhibitiwa kwa sasa havijirudii tena

   Wananchi wa Kijiji cha Uzi wamekiri kupungua kwa Vitendo viovu tangu kuwepo kwa Askari Jamii katika Kisiwa hicho.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.