Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amezindua Sera ya Taifa ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024.
Uzinduzi wa Sera hiyo umefanyika wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo, Waziri Mkuu amesema Tanzania sio mahali sahihi kwa biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya na ametoa wito kwa Vijana kuachana na Dawa za Kulevya zinazoathiri nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania Lyimo Amesema Mapambano ya kukabiliana Kemikali Bashirifu na Operesheni za uteketezaji wa Mashamba ya Bangi bado yanaendelea.
Mhe. Jenister Mhagama -Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya kupiga Vita matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ni wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya Dawa za Kulevya.