WASTAAFU WA JESHI LA POLISI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO

RC KITWANA

    Wastaafu wa Jeshi la Polisi wamesisitizwa kuendelea kutoa mchango wao katika suala zima la Ulinzi na Usalama katika ya Jamii ili kupunguza vitendo vya uhalifu vinavyoendelea Siku hadi Siku.

   Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa ametoa Wito huo katika Sherehe ya kuwaaga Wastaafu 50 wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakifanya kazi katika Vituo mbali mbali vya Mkoa wake.

     Amesema kustaafu ni moja ya taratibu za kiutumishi, hata hivyo Serikali itaendelea kuwatumia kila itakapohitajika kutokana na uzoefu waliyoupata katika kulitumikia Jeshi Taifa.

      Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  na Mkuu wa Operesheni Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar Mathias Nyange

amewashukuru Wastaafu hao kwa kuweza kulitumikia Jeshi hilo kwa uadilifu hadi  kustaafu Wastaafu hao wamesema wako tayari kutoa msaada watakapo hitajika.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.