Waziri Mchengerwa ametoa Maagizo hayo Jijini Dodoma Wakati Akizindua Programu ya uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha ameongeza kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Programu za maboresho ya Serikali za Mitaa tathmini mbalimbali zimebaini kuwepo kwa Changamoto zikiwemo muingiliano wa Majukumu katika Utoaji wa huduma za Kiuchumi na Kijamii baina ya Wizara za Kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Denis Londo, amesema Programu hiyo itaenda kutatua changamoto kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na kuibua vyanzo vipya vya Mapato.
stories
standard