Akifungua Mkutano wa Wadau wa Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Ame Khamis katika Kikao Maalum cha Maelekezo ya Wajibu wa Vyombo vya Habari kuzingatia maudhui na muongozo wakati wa Kuripoti Matukio ya Uchaguzi amesema ni vyema Waandishi Wahabari kufuata Miongozo kama ilivyoekwa wanapofanya Kazi zao.
Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdulla Salim amesema Tume ya Utangazaji Zanzibar ndio Chombo pekee kinacho husika na usajili wa Vyombo vya Habari hivyo Chombo chochote ambacho hakina Leseni na kusajiliwa hakitoruhusiwa kurusha Matukio ya Uchaguzi.
Wakiwasilisha Mada ya wajibu wa Vyombo vya Habari na Muongozo wa Kuripoti Habari wakati wa Uchanguzi Mrajis Tume ya Utangazaji Zanzibar Mohamed Said na Afisa Sheria Tume Utangazaji Khadija Mabrouki wamesema Waandishi wanatakiwa kuandika Habari za ukweli na sahihi ili kuepuka kuleta uchochezi au uvujifu wa amani.
Mrajisi Idara ya Habari Maelezo Jamila Mahmoud Juma amesema Waandishi wa Habari wote wanatakiwa kuwa na Vitambulisho vya Habari Maelezo ambavyo vitamsaidia kuuchukulia Matukio ya Uchaguzi.