WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

WAGENI KUTOKA CHINA

   Wizara ya Fedha na Mipango imesema itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Dhamana na Mikopo kutoka Jamhuri ya Watu  wa China ili kuleta Maendeleo Nchini .

   Akizungumza na Ugeni huo kutokana China Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Sada Mkuya Salum amesema Zanzibar imekuwa na ushirikiano mzuri na Jamhuri ya Watu wa  China katika Sekta mbali mbali ikiwemo Michezo , Habari, Afya pamoja na kuwajengea uwezo Maafisa kwa kuwapatia Mafunzo mabali mbali.

   Katibu Mkuu Afisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt.Juma  Malik Akili amesema wana Miradi mikuu Mitatu ikiwemo ya Barabara , Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Terminal Four pamoja na  wa Bandari Mpya ya Mangapwani .

   Nao Ugeni kutoka Jamhuri ya China wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuhakikisha wanatimiza malengo yaliokusudiwa .

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.