Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson, amesema amani, tulivu na usalama ndio ngao ya Nchi za Afrika na Duniani kote.
Akizungumza katika muendelezo ya Ziara yake na Wabunge wa Mabunge Duniani, amesema Nchi nyingi Barani Afrika zina Migogoro na vita vya Wenyewe kwa Wenyewe na kusababisha athari mbali mbali.
Amesema Umoja huo unakusudia kujadili Maeneo yote yenye matatizo mbali mbali ikiwemo vita na kuyatafutia ufumbuzi.
Aidha Dkt.Tulia, ametoa Pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kutokana na kuwepo mazingira mazuri pamoja na Maeneo ya Kihistoria.
Nao Wabunge hao wamesema wamefurahishwa na ukarimu, amani na utilivu uliopo Zanzibar.
Lengo laZiara ya Ujumbe huo ni kuhamasisha Utalii kwa Wageni kuja Kutembelea Zanzibar ili kuona Vivutio vya Utalii.