ZIC IKISHIRIKIANA NA MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION WAKABIDHI MSAADA WA VITABU KWA MKOA WA KUSINI UNGUJA

ZIC NA  TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION

   Shirika la Bima Zanzibar ZIC likishirikina na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Fondation wamekabidhi msaada wa Vitabu vya Mitaala kwa Skuli za Secondari ili kukuza kiwango cha ufaulu katika Skuli za Mkoa ya Kusini Unguja. 

   Akikabidhi  Vitabu vya Mitaala kwa Skuli  za Sekondari,  Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ndg.Jape Ussi Khamis amesema Elimu ndio msingi wa maendeleo katika Nchi hivyo ni vyema kwa Jamii kuunga Mkono jitihada za Serikali katika kuendeleza upatikanaji wa Elimu bora. 

    Amesema Shirika la Bima litaendelea kushirikiana na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali ili kuona malengo  ya kuimarisha Sekta ya Elimu Nchini  yanafanikiwa  kwa kukuza Kiwango cha Ufaulu kwa Wanafunzi.

   Mkurugenzi Mtendaji Sabra Mohamed kutoka  Mwanawake Initiatives Fondation amesema moja ya Vipaumbele vya Taasisi hiyo  ni kuhakikisha wanasaidia jitihada za upatikanaji wa Elimu bora kwa  kuweka Miundombinu imara na endelevu  kwa Vijana ili waweze kufikia malengo yao na Taifa kwa Ujumla.

   Afisa huduma za Wanafunzi Idara ya Elimu Sekondari Bi.Rukia Ramadhani amesema Wizara ya Elimu bado inahitji Vitabu kwa Maendeleo ya Wanafunzi hivyo amewataka Wadau kuendelea kuchangia ili kukuza Maendelo ya Elimu Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.