Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Fedha. Za Bajeti ya Serikali kuangalia Vipaumbele vya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara ,Maji pamoja na Uimarishaji wa uendelezaji wa Viwanja. Vya Ndege.
wamesema ili mambo hayo yaweze kufanikiwa Wajumbe hao wameishuri Serikali kuingiza Fedha za Bajeti kwa Wakati ili ziweze kuharakisha maendeleo ya haraka hasa katika upatikanaji wa huduma ya Maji la muda mrefu.
Wajumbe hao wametoa michango hiyo wakati wakijadili mpango wa Maendeleo ya wa Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025 katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani.
Wameisisitiza Serikali kuharakisha kuelekeza nguvu zake katika suala la uchimbaji wa Mafuta na Gesi kwa kuwa na Bajeti ya Fedha za kutosha kuhakikisha Nishati hyo inafanikiwa.
Wakichangia Sekta ya uwekezaji Wajumbe hao wamesema bado kuna Visiwa ambavyo ni Vivutio vya Utalii walivopewa wawekezaji ambavyo hadi sasa havija endelezwa hivyo vinahitaji kuangaliwa upya na Serikali kwa kuvifanyia maamuzi
Wameishauri Serikali kuboresha Mifumo ya Fedha ya ndani ili kupunguza upotevu wa Fedha pamoja na kupunguza misamaha ya Fedha za Kodi kwa Wafanyabiashara.