Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mhe Dkt.Saada Mkuya Salum katika Baraza la Wawakilishi ametoa ufafanunuzi wa bajeti katika Sekta mbalimbali za Serikali.
“Baraza la Wawakilishi liliridhia mapendekezo ya Serikali kwa kutoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa Miradi ya Nyumba Nafuu (Affordable Housing Scheme) ili kuimarisha makaazi bora kwa wananchi pamoja na kupunguza gharama za ununuzi wa nyumba hizo”
“Hadi kufikia Machi, 2024, miradi miwili imenufaika na unafuu huo ikiwemo; Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Bei Nafuu katika Mji wa Dkt. Hussein Mwinyi eneo la Uwanja wa Magereza, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na Mradi wa Nyumba za Makaazi Mombasa unaojengwa” .
stories
standard