Wanafunzi wanaoshiriki Mashindano ya umitashumta Kanda ya Unguja na Pemba wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika Michuano hiyo inayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwenye Ziara ya kuwatembelea Washiriki hao kwa lengo la kujua matokeo ya michezo yao na changamoto zinazowakabili.
Nae Mkurugenzi wa Wizara ya ELimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Hafsa Abodtwalib amesisitiza Washiriki hao kuhakikisha wanatunza nidhamu zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umitashumta Kanda ya Pemba Ismail Alhamad amewatoa shaka Wazanzibari kwa kuhakikisha watadumisha umoja na Mshikamano na kuludi na Makombe Visiwani humo.
stories
standard