SMZ INATHAMINI UHUSIANO WA VILABU KATIKA KUIMARISHA MUUNGANO

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema ushirikiano uliopo baina ya Timu ya Mpira ya Baraza la Wawakilishi na Timu ya Arusha Wazee Club umekuwa ukitoa fursa mbali mbali wanapotembeleana ikiwemo kujifunza Kilimo, Utalii  na kuimarisha  Afya kupitia  Michezo na kuimarisha Muungano kivitendo.

    Akizingumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu hizo katika Hafla ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Viwanja  vya Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar.

   Amesema Serikali inathamini uhusiano unaofanyika baina ya Taasisi, Jumuia na Vilabu vya Michezo kwa pande zote za Muungano kutokana na mchango mkubwa wa kimaendeleo unaopatikana kupitia Mashirikiano hayo.

   Aidha Mhe.Hemed amewataka wenye Viti wa Timu hizo Mbili kuendelea kuwaongoza vizuri Wanachama wao na kuhakikisha wanauendeleza umoja wao ambao una mchango mkubwa katika kuimarisha na kudumisha Muungano uliotimiza Miaka Sitini(60) tangu kuasisiwa kwake.

    Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid amepongza  uhusiano wao uliodumu kwa muda mrefu ambao umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa pande zote mbili.

    Mwenyekiti Mwenza kutoka Timu ya Arusha Wazee Club Ndugu Ally Mamuya amesema ushirikiano kati ya Timu hizo Mbili umekuwa ni wa muda mrefu ambao umekuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kufanya Mazoezi ya pamoja kwa kuimarisha Afya ya Mwili na Akili pamoja na kuzidi kuendelea kuutangaza Utalii kati ya Zanzibar na Arusha.

   Nae  Mwenyekiti wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Sports Club Mhe.Miraji Khamis Mussa (Kwaza) ametoa shukran kwa Mabenki mbali mbali hapa Nchini kwa kuwapatia ushirikiano mkubwa katika kufanikisha shughuli mbali mbali za Baraza la  Wawakilishi ikiwemo  suala zima la Michezo ambalo huwajenga zaidi kiafya.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.