Kijana anaefahamika kwa Jina la Nada Faki Khamis Mwenye Umri wa Miaka Thelathini na Nane Mkaazi wa Kinyasini Wilaya ya Kaskazini 'a' Mkoa Kaskazini Unguja amekutwa akielea katika Bwawa la Maji la Banda Maji Akiwa Amefariki Dunia
Akithibisha kutokea kwa Tukio hilo Kamanda wa Kikosi cha Zima Moto na Uokozi Mkoa Kaskazini Unguja Kamanda Asha Othman amesema Mnamo Majira ya Saa Saba na Nusu za Mchana walifanikiwa kupata Taarifa ya Mtu Akielea katika Bwawa la Maji Maeneo ya Banda Maji na kufanya juhudi za uokozi Majira ya Saa Nane na walifaniwa kuupata Mwili wa Marehemu ambao umeshaaza kuharibika na kuupeleka katika Hospital ya Wilaya ya Kivunge kwa ajili ya Uchunguzi
Kufuatia Tukio Mkuu wa Wilaya Kaskazini 'a' Othman Ali Maulid alifika katika Eneo hilo na amewataka Wananchi kuwa makini wakati wanapofanya Shughuli zao katika Mito na Mabwawa mbali mbali ili kujiepusha na Matukio ya aina hiyo