WATUHIMIWA 251 WAKAMATWA KWA VITENDO VYA UHALIFU MKOA WA MJINI MAGHARIB

MKOA WA MJINI MAGHARIB

     Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amesema jumla ya watuhumiwa 251 wamekamatwa kufuatia operesheni maalum ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa Nchini.

       Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Vuga wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.

     Amesema watuhumiwa waliokamatwa 22 wamekamatwa na mapanga na vifaa vya kuvunjia nyumba, 20 wamekamatwa kwa makosa ya unyan’ganyi, kujeruhi na kushambulia, 6 kwa makosa ya wizi wa pikipiki wakiwemo mafundi wa pikipiki wanaopokea mali za wizi na watuhumiwa 203 wamekamatwa kwa makosa ya uzembe na ukorofi.

      Aidha, amefahamisha watuhumiwa wote waliokamatwa katika operesheni hiyo watafikishwa katika vyombo vya sheria na majalada yao yemeshafunguliwa kwa ajili ya kufikishwa katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ili kuendelea na taratibu nyengine za kisheria.

       Nae Mkuu wa Wilaya Magharibi ‘B’ ambae ni Kaimu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Hamida Mussa Khamis ameishukuru Kamati ya Usalama wa Mkoa kwa kuendelea kuzisimamia Wilaya zao na kutoa muongozo wa jinsi ya kukabiliana na uhalifu huo.

        Akielezea wilaya yake amesema kuwa bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa na vikundi vya uhalifu ikiwemo Kinuni Kwarara Hawai pamoja na Mchikichini.

       Kwa upande wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ACP Richard Thadei Mchomvu amesema operesheni huo imefanyika kwa aina yake jambo ambalo limesaidia kuleta mafanikio ya kuwakamata wahalifu.

      Mali zilizookolewa katika Operesheni hizo ni pikipiki 14, Televisheni 4 , simu 16, mifuko ya saruji 4, Tiles box 5, Viatu vya raba pair 6 , pasi za umeme 3, frame 44 za pikipiki aina ya klick na vespa pamoja na N’gombe 2.

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.