Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mtama mkoani Lindi, ameendesha zoezi la harambee kwa lengo la kupata nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake katika Halmashaur ya Mtama
Hii ni kutokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan , kuwa Viongozi wa Chama wanatakiwa wawe na nyumba Kwa ajili ya makazi
Katibu wa (UWT) Mtama ameshirikiana na Viongozi mbalimbali katika harambee hio akiambatana na Mbunge wa kuteuliwa Mkoani Lindi katika Jimbo la Mchinga, Bi Ridhiki Lulindi aliewakilishwa na Mwenyekiti wa (UWT) Mtama, Bi. Bibie Rashid Magomba
Aidha, Katyale amewashukuru UWT waliojitokeza katika harambee hio kwani walifanikiwa kukusanya mil.1007000 ahadi, milioni 2,500,000 na mifuko 3 ya saruji
Aidha Katyale alieleza lengo nikupata miliioni 25,000,000 kuweza kukamilisha zoezi Hilo.
Kwa upande wa Madiwani wa Mtama ,Bi Mariam Petro Nyale ambaye ni Diwan kata ya Mtama alimshukuru Katyale kwa kuendesha harambee hio kwani haijawahi kutokea katika UWT Lindi.
Pia Katyale amewaomba wadau kujitokeza kusaidia ujenzi wa nyumba hiyo.