WIZARA YA UCHUMI WA BLUU KUFANYA UTAFITI WA SUMU YA KASA

Barazani

    Wizara ya Uchumi wa Bluuu na Uvuvi   imepanga kufanya utafiti juu ya Sumu Asili ambayo imo ndani ya Mwili wa Kasa. 

imesema  imeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuzitambua Sumu  zilizomo ili kujua athari zake . 

    Akijibu Swali la  Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani  Mhe.Mussa Foum Mussa  Waziri wa Wizara hiyo amesema  Elimu itakayopatikana kutokana na utafiti huo itatumika katika kuelimisha Jamii juu ya athari zitonazo na ulaji wa Kasa . 

    Amesema Wizara inaendelea kuchukua hatua kwa Wavuvi  ambao  wanaendelea kujishughulisha  na Uvuvi wa Viumbe hao. 

     Wakati huo huo  Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe.Shamata Shaame Khamis amesema Kilimo cha Kisasa kina mchango mkubwa wa kuwakomboa Wakulima  iwapo maeneo yatapatiwa Teknolojia za Kisasa  kwa kuzalisha Mazao yenye tija kwa Eneo Dogo. 

     Wajumbe wa Baraza la Wawaakilishi  wamepitisha Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora  kwa Mwaka wa Fedha  2024/2025.

    Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais ,Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.