MAKAMU WA RAIS AMETOA MAAGIZO KUIMARISHA SEKTA YA ASALI NCHINI

MAKAMO WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Philip Mpango, ametoa maagizo mbalimbali   yatakayosadia kuimarisha sekta ya asali Nchini ikiwemo Balozi zote kujidhatiti kutafuta Masoko ya Bidhaa zinazotokana na Nyuki ili kusaidia Taifa kupata Fedha za Kigeni na kujimarisha Kiuchumi.

Dk.Mpango ametoa  maagizo hayo  wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma.

Aidha Dkt.Mpango ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta hiyo kuja na mpango maalum wa Ufugaji wa Nyuki.

Awali, Waziri wa maliasili na Utalii,Mhe. Angelah Kairuki amesema Sekta hiyo kupitia Nyuki imekuwa na mchango mkubwa katika eneo la uzalishaji wa Mazao ya Chakula.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.