ZANROD KUJENGA MTARO WA KUPITISHIA MAJI YA MVUA KUMVUNI PUJINI

Mitaro Pemba

   Wakala wa Barabara Zanzibar Ofisi ya Pemba, imetekeleza agizo la Viongozi Wakuu wa Kitaifa, la Kujenga Mtaro wa kupitishia maji ya Mvua eneo la Kumvuni Pujini.

     Hayo yameelezwa na Injinia Said Rashdi Said kutoka Wakala wa Barabara Pemba, wakati wa Ukaguzi wa Mtaro huo ambao ulikua ni kilio kikubwa kwa Wananchi wa Eneo hilo.

     Amesema lengo la Wakala ni kutatua Kero mbali mbali za Wananchi,na tayari juhudi hizo zimechukuliwa kwa Vitendo na baada ya Mwezi Mmoja ujao Mtaro huo utakua umeshakamilika.

     Mmoja ya Wananchi wa Kumvini Pujini Ndg.Iliyasa Juma Amour, amesema Mtaro huo ulikua kilio cha muda mrefu, na wameshukuru kwa kujengwa mtaro huo.

      Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandisi Cosmos Masolwa, amesema lengo la kujengwa kwa Mitaro hiyo ni kuondosha kero za Wananchi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.