Watu 11 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili kugongana katika eneo la Somanga Wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Akizungumza leo Jumatatu Aprili 22 ,2024 kamanda wa polisi mkoa wa Lindi John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 07:30 eneo la Somanga kata ya Somanga Tarafa ya Miteja halmashauri ya Kilwa Mkoani Lindi barabara kuu ya Lindi- Kibiti ikihusisha Gari lenye namba za usajili T224DZT HOWO ikiwa na tela namba T920 CUK Mali ya Specialised Hauliers ikitokea Dar es salaam likigongana na gari lenye namba za usajili T707 DSX Mazda Min Bus inayomilikiwa na Hashimu Daudi akitokea Somanga kuelekea Nangurukuru
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni Matumizi mabaya ya Barabara kwa Dereva wa Gari Namba T224 DZT HOWO Ikikokota tela lenye Namba T920 CUK aitwaye Abdallah Hamisi
Majeruhi wote nane wamepelekwa katika hosptali ya Tingi kwaajili ya matibabu zaidi huku miili ya marehemu ikiwa tayari imekabidhiwa kwa ndugu tayari kwa taratibu za mazishi