Akizungumza walipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania wakiongozana na Watendaji wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Yahya Rashid Abdallah amesema usalama wa Anga unatakiwa kupewa kipaumbele ili kuiwezesha Anga kuwa salama na kuleta tija.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri Tanzania TCAA Daniel Malanga amesema wanaendelea kuimarisha miundombinu kwa mustakabali wa maendeleo ya Usafiri na usafirishaji kwa njia ya Anga ili kuweza kudhibiti usalama .
Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi ipo Tanzania Bara kwa ajili ya shughuli za kawaida za Kamati hiyo.
stories
standard