Ofisi ya Mufti Zanzibar imewaomba Wananchi kuhudhuria katika Ibada ya sala ya eid na baraza la eid ili kusikiliza nasaha na Miongozo itakayotolewa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussen Ali Mwinyi.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Khalid Ali Mfaume amesema Siku ya Eid ni muhimu kukumbushana mambo yanayohusu Dini ya Kiislamu na kukatazana mabaya ili kuepusha Jamii kwenda kinyume na Maadili yao
Akizungumzia kuhusu Kuandama kwa Mwezi Katibu Khalid amesema Skukuu hiyo itasherehekewa kulingana na kuandama kwa Mwezi hivyo amewaomba Wananchi kuwa na ushirikiano katika kufuatilia Taarifa za kuandama kwa Mwezi Mpya wa Kiislamu.
stories
standard